• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Mchumi wa Kenya asema sera ya kujilinda kibiashara ya Marekani haina manufaa kwa upande wowote

  (GMT+08:00) 2018-03-30 16:44:21

  Rais Donald Trump wa Marekani hivi karibuni alitangaza mpango wa kuongeza ushuru wa dola za kimarekani bilioni 60 dhidi ya bidhaa zinazoagizwa kutoka China, na kuzuia uwekezaji wa kampuni za China nchini Marekani, hatua ambayo imefuatiliwa duniani nzima. Alipohojiwa na mwandishi wetu wa habari, mchumi maarufu wa Kenya Anzetse Were amesema sera ya kujilinda kibiashara haisaidii upande wowote, na nchi za Afrika zinatetea sera ya biashara huria na kupenda kushirikiana na China.

  Bibi Anzetse Were alisema kuanzisha vita ya biashara dhidi ya China ni utendaji usiowajibika wa Marekani kwa uchumi wa dunia nzima, na Marekani nayo itaumia yenyewe. Anasema,

  "hatua hiyo ya Marekani itasababisha athari mbaya kwa pande mbalimbali sio China peke yake. Kwa mfano vipuri vya baadhi ya bidhaa za kielektroniki zinazoagizwa nchini Marekani kutoka China huwa vinatolewa na nchi na sehemu mbalimbali, si za Asia tu bali pia Ulaya. Kama Marekani inaongeza ushuru dhidi ya bidhaa hizo, nchi na sehemu zote zilizopo kwenye mtiririko huo wa utoaji zitaathiriwa. Kwa upande mwingine, wateja nchini Marekani pia watadhurika kimaslahi, kwani bidhaa za China zina soko kubwa nchini Marekani, na kuongeza ushuru dhidi ya bidhaa za China kutasababisha kuongezeka kwa bei ya bidhaa hizo wanazotumia wateja wa Marekani, na kampuni za Marekani zinazoagiza bidhaa kutoka China pia zitapata hasara kubwa."

  Bibi Anzetse anaona sababu kuu ya kuongezeka kwa mvutano wa biashara kati ya China na Marekani ni kutokuwa na uwiano wa biashara kati ya nchi hizo mbili. Marekani inaitupia lawama China kutokana na urari mbaya wa kibiashara kati yao, lakini hali halisi ni kuwa kukosekana kwa uwiano wa mtindo wa kibiashara ndio sababu kuu. Anasema tatizo hilo haliwezi kutatuliwa kwa njia ya kuongeza ushuru, na Marekani inapaswa kutatua matatizo yake yenyewe badala ya kushambulia nchi nyingine. Anasema,

  "Sababu kuu ya tatizo hilo ni baadhi ya bidhaa za Marekani zinakosa ushindani ikilinganishwa na bidhaa za China, na badala ya kutumia njia ya kuongeza ushuru, Trump anapaswa kufikiria jinsi ya kupanga mpango wa muda mrefu wa kuongeza ushindani wa bidhaa za Marekani."

  Bibi Anzetse amesema sera ya kujilinda kibiashara itarudisha nyuma maendeleo ya nchi, na ni mazingira huria pekee yanaweza kuingiza uhai kwa biashara ya pande mbili. Sera ya mambo ya nje ya China inayotetea kufungua mlango inalingana na mkondo wa zama za leo, na kwamba nchi za Afrika zilizopo kwenye kipindi muhimu cha maendeleo zinataka kutimiza biashara huria, na kuboresha mpangilio wa raslimali. Ameeleza matumaini yake kuwa kampuni za China zitawekeza zaidi barani Afrika, kuleta hamasa kwa kampuni za Afrika, na kuhimiza maendeleo ya viwanda na uzalishaji. Anasema,

  "Tofauti na sera ya kujilinda kibiashara inayotekeleza Marekani, Afrika inataka sana kutimiza biashara huria. Tumetoa mchango wetu kwa biashara ya kimataifa, na vilevile tunapenda kuona pande nyingine zikiunga mkono maendeleo yetu ya viwanda na uzalishaji. Tunakaribisha kampuni za China kuwekeza barani Afrika, kusaidia sekta ya viwanda na kuboresha muundo wa kiuchumi. Ujio wa kampuni za China kwenye soko la Afrika utaleta shinikizo kwa kampuni za Afrika, lakini hatupaswi kuzuia ujio wao, badala yake ni kufikiria jinsi ya kuongeza ushindani wa kampuni za Afrika. Naona sasa uhusiano kati ya China na Afrika uko katika kipindi kizuri, na hakika utaendelezwa kwenye ngazi ya juu zaidi."

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako