• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Marekani yasema huenda itawafukuza wanadiplomasia zaidi wa Russia

    (GMT+08:00) 2018-03-30 17:23:28

    Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Marekani Bi. Heather Nauert amesema, nchi hiyo imesikitishwa na hatua ya Russia kuwafukuza wanadiplomasia 60 wa Marekani, na huenda Marekani itawafukuza zaidi wanadiplomasia wa Russia.

    Wizara ya mambo ya nje ya Russia jana ilitangaza kuwa, naibu waziri mkuu wa nchi hiyo Bw. Sergei Ryabkov alikutana na balozi wa Marekani nchini humo Bw. John Huntsman, na kumweleza kuwa Russia itawafukuza wanadiplomasia 60 na kufunga ubalozi mkuu wa Marekani ulioko Saint Petersburg.

    Habari nyingine zinasema, katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Antonio Guterres jana alionya kuwa, uhusiano kati ya Marekani na Russia unarudi kwenye hali ya wasiwasi kama kipindi cha Vita Baridi, na ana wasiwasi wa ukosefu wa utaratibu wa kusuluhisha hali hiyo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako