• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yaanza sensa ya pili ya kitaifa kuhusu vyanzo vya uchafuzi

    (GMT+08:00) 2018-03-30 18:07:47

    China itafanya sensa ya pili ya kitaifa kuhusu vyanzo vya uchafuzi mwaka huu, ikiwa ni miaka 10 baada ya sensa ya kwanza kufanyika.

    Mkurugenzi wa idara inayosimamia sensa iliyopo chini ya Wizara ya Ikolojia na Mazingira ya China Hong Yaxiong amesema, sensa hiyo ni ishara ya kazi za kimsingi za ulinzi wa mazingira zinazofanywa na China. Amesema vyanzo vikubwa vya uchafuzi vitahakikiwa na kuwekwa kwenye kumbukumbu, ikiwa ni sehemu ya ushahidi kwa watunga sera kusimamia na kuboresha mazingira, na pia kuzuia hatari.

    Kazi ya kuchunguza kiwango, utaratibu, na mgawanyiko wa vyanzo vya uchafuzi itamalizika mwaka huu na matokeo yatatangazwa mwaka ujao.

    Utafiti wa awali umegundua vyanzo vya uchafuzi katika viwanda karibu milioni 7.4 na maeneo ya kilimo milioni moja, pamoja na kuongezeka kwa vyanzo vinavyotokana na makazi ya binadamu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako