• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Umoja wa Mataifa wasifu nafasi ya China katika kusuluhisha suala la Peninsula ya Korea

    (GMT+08:00) 2018-03-30 18:08:27

    Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema China ni mchango muhimu katika suluhisho la suala la Peninsula ya Korea.

    Bw. Guterres amesema hayo jana kwenye makao makuu ya Umoja huo mjini New York, Marekani, na kuongeza kuwa ametiwa moyo na ziara ya hivi karibuni ya kiongozi wa Korea Kaskazini nchini China. Pia amesema hivi sasa kuna fursa ya suluhisho la amani katika kitu ambacho miezi michache iliyopita ilikuwa tishio kubwa kwa dunia.

    Katibu mkuu huyo ameweka matumaini makubwa katika mikutano ijayo ya Korea Kusini na Korea Kaskazini na pia Korea Kaskazini na Marekani, akisema kuanza tena kwa mazungumzo ya Korea na majadiliano kati ya Korea Kaskazini na Marekani ni jambo linalohitajika kwa sasa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako