• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ethiopia yauza dhamana kwa raia wake wanaoishi ugenini ili kufadhili ujenzi wa bwawa

    (GMT+08:00) 2018-03-30 18:51:10

    Ethiopia imeuza dhamana zenye thamani ya dola za kimarekani milioni 56 kwa raia wake wanaoshi ugenini ili kufadhili ujenzi wa bwawa la umeme linalojengwa kwenye Mto Nile.

    Msemaji wa Wiara ya Mambo ya Nje ya nchi hiyo Meles Alem amesema, kutokana na mauzo ya dhamana hizo, Ethiopia inalenga kuwajumuisha raia wake wanaoishi nchi za nje kwenye zoezi la ujenzi wa taifa.

    Tayari Ethiopia imekusanya dola milioni kadhaa kutoka kwa wananchi nchini humo ili kufadhili ujenzi wa bwawa hilo ambao unatarajiwa kugharimu dola za kimarekani bilioni 4.7. Bwawa hilo linatarajiwa kutoa megawati 6,450 za umeme litakapokamilika.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako