• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Bandari kubwa zaidi kusini mwa Jangwa la Sahara yaanza kujengwa nchini Nigeria

    (GMT+08:00) 2018-03-30 18:51:48

    Mradi wa ujenzi wa Bandari ya Lekki ambayo ni kubwa zaidi kusini mwa Jangwa la Sahara na yenye kina kirefu umezinduliwa mjini Lagos, kusini magharibi mwa Nigeria.

    Hafla ya uzinduzi huo ilihudhuriwa na Makamu wa Rais wa Nigeria Bw. Yemi Osunbajo, pamoja na maofisa wengine wa serikali ya nchi hiyo, pia balozi mdogo wa China aliyeko mjini Lagos, Nigeria Bw. Chao Xiaoliang, na mwenyekiti wa kampuni ya uhandisi wa bandari ya China inayojenga ujenzi huo Bw. Lin Yichong.

    Katika hafla hiyo, Bw. Osunbajo amesema mradi huo ni wa kihistoria na eneo la biashara huria la Lekki linalouza bidhaa kwa wingi nje ya nchi litafaidika zaidi kutokana na bandari hiyo.

    Naye waziri wa uchukuzi wa Nigeria Bw. Rotimi Amaechi amesema baada ya kukamilika kwa ujenzi huo, meli kubwa zitaweza kuingia katika bandari hiyo moja kwa moja.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako