• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ziara ya rais wa Zimbabwe nchini China kutia nguvu mpya ya kuhimiza maendeleo ya uhusiano kati ya nchi hizo mbili

    (GMT+08:00) 2018-03-30 19:12:30

    Rais Emmerson Mnangagwa wa Zimbabwe atafanya ziara nchini China kuanzia Aprili 2.

    Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bw. Lu Kang amesema, ziara hiyo itatia nguvu mpya katika maendeleo ya uhusiano kati ya nchi hizo mbili. Amesema, China inatilia maanani maendeleo ya uhusiano kati ya nchi hizo mbili, na kupenda kufanya juhudi pamoja na Zimbabwe kuzidi kuinua kiwango cha uhusiano huo, ili kunufaisha zaidi nchi hizo mbili na watu wake.

    Ujenzi wa mradi wa upanuzi wa kituo cha uzalishaji wa umeme kwa nishati ya maji kilichoko kusini mwa Mto Kariba uliojengwa kwa mkopo wa China umekamilika. Bw. Lu amesema, mradi huo utatoa mchango katika ongezeko la utoaji wa umeme nchini Zimbabwe na kuhimiza maendeleo ya uchumi na jamii ya nchi hiyo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako