• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wakulima Kenya walalamikia uhaba wa mbolea

    (GMT+08:00) 2018-03-30 19:25:02

    Wakulima wa nafaka kutoka eneo la kaskazini mwa Rift valley wamelalamikia uhaba wa mbolea msimu huu wa upanzi. Wakulima hao wamesema uhaba wa mbolea unahatarisha kupatikana kwa chakula cha kutosha nchini Kenya.Mkurugenzi wa shirikisho la wakulima Bw Kipkorir Menja amesema wakulima waliofika katika bohari ya bodi ya kitaifa ya mazao na nafaka walipigwa na butwaa baada ya kufahamishwa kuwa maghala hayo hayakuwa na mbolea. Wakulima hao wametaka kujua sababu ya mbolea hiyo kukosekana wakati huu na kushuku kuwa huenda kuna njama ya kuficha mbolewa hiyo ili wafanyabiashara wachache wauzie wakulima kwa bei ghali. Menjo ameitaka serikali kuelezea wakulima ilikokwenda mbolea ambayo ilidaiwa kufika katika bandari ya Mombasa mwezi uliopita.Aidha wakulima hao pia wamelalamikia msongamano na foleni ndefu za kuuza mahindi katika NCPB.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako