• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • TRA yakamata majahazi manne ya bidhaa za magendo

    (GMT+08:00) 2018-03-30 19:25:25

    Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kwa kushirikiana na maofisa wa Polisi imekamata majahazi manne yenye bidhaa mbalimbali katika wilaya ya Muheza kwa kupitia njia ya magendo zikitokea visiwani Zanzibar.

    Meneja wa Forodha wa TRA mkoani Tanga Edward Ndupa amesema bidhaa zilizokamatwa ni tani tano za sukari, vitenge, khanga na mafuta ya kula madumu 470 ya lita 20 kila moja.

    Ndupa ameongeza kuwa mpaka sasa wafanyabiashara wenye bidhaa hizo hawajafahamika, hivyo mamlaka hiyo inafanya utaratibu wa kuzitaifisha moja kwa moja bidhaa hizo.

    Kamanda wa Polisi mkoani hapa, Edward Bukombe aliwataka wafanyabiashara wote wanaojihusisha na biashara za magendo kuacha mara moja vitendo hivyo.

    Aliongeza kuwa, polisi wataendelea kushirikiana na TRA, kuwakamata wote wanaosafirisha bidhaa kupitia njia sizizo rasmi.

    Amewataka wafanyabiashara wote wanaokwepa kulipa kodi na kupitisha bidhaa zao katika njia za magendo kuacha mara moja tabia hiyo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako