• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Nauli yapanda kwa abiria wakati huu wa pasaka

    (GMT+08:00) 2018-03-30 19:25:44

    Wahudumu wa usafiri wa umma katika maeneo mbalimbali nchini Kenya walianza kutekeleza nyongeza ya nauli kwa kati ya asilimia 20 na 60 kwa wasafiri wanaoelekea vijijini kujumuika na wapendwa wao katika sherehe za Pasaka.

    Abiria waliokuwa wakisafiri hadi Murang'a kutoka Nairobi walijipata wakitozwa nauli ya shilingi 250 badala ya ile ya kawaida ya Sh150 na Sh200, huku wale wa Nyeri walijipata wakitozwa kati ya Sh350 na Sh400 na wengine wa miji kama Nakuru, Naivasha, Nanyuki, Nyahururu na Meru wakijipata taabani.

    Mwenyekiti wa muungano wa wamiliki magari katika eneo la Mlima Kenya, Micah Kariuki amesema kuwa wingi wa watu waliokuwa wakisaka huduma za usafiri ndio ulikuwa ukiweka nauli ya kutozwa.Ameongeza kuwa pia bei ya mafuta imepanda na hivyo basi kuchochea nyongeza ya nauli. Alisema kuwa uchumi wa Kenya kwa sasa hauna uwezo wa kuzua msismko wa sherehe "kwa kuwa kila mtu analia kuhusu ugumu wa maisha

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako