• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Pato la taifa Tanzania laendelea kuimarika

    (GMT+08:00) 2018-03-30 19:26:02

    Kufuatia kuongezeka kwa shughuli za kiuchumi nchini Tanzania, pato la Taifa limeendelea kuwa imara na kuongezeka kutoka shilingi trilioni 61.4 mwaka 2012 hadi kufikia shilingi trilioni 103.7 mwaka 2016.

    Kwenye mikoa ya Nyanda za Juu Kusini, pato liliongezeka kutoka shilingi trilioni 9.8 mwaka 2012 hadi kufikia shilingi trilioni 16.6 huku mkoa wa Rukwa pato liliongezeka hadi kufikia shilingi trilioni 3.7 kwa mwaka juzi.

    Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi wa Idara ya Uchumi Benki Kuu Nyanda za Juu Kusini, Sungura Mashini.

    Sungura amesema kwa mikoa ya nyanda za juu kusini, wastani wa pato la mtu mmoja liliongezeka kutoka shilingi milioni 1.4 mwaka 2012 na kufikia shilingi milioni 2.5.

    Kwa mkoa wa Rukwa, wastani wa pato la mtu mmoja uliongezeka na kufikia Sh milioni 2.1 kwa mwaka 2016.

    Amesema, mfumuko wa bei kikanda, ulizidi kupungua kutoka asilimia 6.9 Juni 2016 na kufikia asilimia 1.5 Desemba mwaka 2017.

    Kushuka kwa mfumko wa bei, kulichangiwa na kushuka kwa bei za mazao ya chakula.

    Bei ya mahindi na viazi mviringo, zilishuka huku bei ya mchele na maharage zkipanda.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako