• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Idadi ya wanafunzi wa China wanaosomea nchi za nje yazidi laki 6 mwaka jana

    (GMT+08:00) 2018-03-30 19:32:20

    Wizara ya elimu ya China imesema, mwaka jana idadi ya wanafunzi wa China waliosomea nchi za nje ilizidi laki 6 kwa mara ya kwanza, ambayo iliongezeka kwa asilimia 11.74 kwa kulinganishwa na mwaka juzi, hivyo China kudumisha hadhi ya nchi yenye wanafunzi wengi zaidi wanaosomea nchi za nje duniani.

    Takwimu zimeonesha kuwa, wakati idadi ya wanafunzi wanaosomea nchi za nje ikiongezeka, watu wenye ujuzi wa hali ya juu wameonesha mwelekeo wa kurudi nchini. Mwaka jana, wanafunzi laki 4.8 waliosoma nchi za nje walirudi nchini China, ambao idadi ya watu wenye shahada ya uzamili na uzamifu au baada ya shahada ya uzamifu imefikia laki 2.3 ikiongezeka kwa asilimia 14.9 ikilinganishwa na ya mwaka juzi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako