• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ofisi ya siasa ya kamati kuu ya chama cha CPC yafanya mkutano

    (GMT+08:00) 2018-03-30 19:32:57

    Ofisi ya siasa ya kamati kuu ya chama cha kikomunisti cha China CPC imefanya mkutano na kusikiliza ripoti kuhusu tathmini ya kazi za kupambana na umaskini ya kamati za chama na serikali za mikoa, na kutoa matakwa ya kufanikisha kazi hiyo.

    Mkutano huo ulioongozwa na Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya CPC Xi Jinping, unaona kuwa mwaka jana mpango uliowekwa na kamati hiyo kuhusu kazi ya kuondoa umaskini umetekelezwa kwa pande zote, majukumu ya idara mbalimbali za sehemu mbalimbali yameimarika, na utaratibu wa makatibu wakuu wa kamati za chama za ngazi tano kuwajibika na kazi ya kuondoa umaskini umeundwa. Pia sera ya kupunguza umaskini kwa hatua za kulenga imepata mafanikio, kazi ya kupunguza umaskini kwa uratibu kati ya sehemu ya mashariki na ya magharibi imeharakishwa, na kazi hiyo imeinuliwa kwenye kiwango kipya.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako