• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa Namibia asema ushirikiano kati ya China na Afrika una manufaa kwa pande zote mbili

    (GMT+08:00) 2018-03-31 18:20:36

    Rais Hage Geingob wa Namibia amesema, kuimarishwa kwa uhusiano kati ya Namibia na China kunathibitisha kuwa ushirikiano kati ya China na Afrika unanufaisha pande zote mbili, akisitiza kuwa maneno yoyote yanayolaani uwekezaji wa China barani Afrika au kukashifu ushirikiano kati ya China na Afrika hayatakiwi kuvumiliwa. .

    Rais Geingob ambaye yuko ziarani nchini China kutokana na mwaliko wa rais Xi Jinping wa China aliyasema hayo jana ambapo pia aliongeza kuwa, China ni rafiki wa daima wa Namibia, hivyo kuimarishwa kwa uhusiano kati ya pande hizo mbili kutahimiza ushirikiano kuelekea kwenye kipindi kipya, na yafaa kuwapinga watu wanaojaribu kukashifu ushirikiano kati ya China na Afrika. Pia alisema kuwa China iliwekeza barani Afrika kutokana na mahitaji ya nchi za Afrika na haikuweka sharti lolote, na ushirikiano kati ya pande hizo mbili ni wa usawa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako