• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mji mkongwe wa London wapenda kuunga mkono ujenzi wa eneo jipya la Xiong'an China kwa teknolojia za kisasa

    (GMT+08:00) 2018-04-01 12:45:46

    Meya wa mji mkongwe wa London Bw. Charles Bowman amesema mji wake una uzoefu mwingi katika kujenga mji wenye teknolojia za kisasa, na unapenda kuunga mkono ujenzi wa eneo jipya la Xiong'an China kwa teknolojia za kisasa na kwa njia isiyochafua mazingira. Hivi karibuni Bw. Bowman akiongoza ujumbe wa kibiashara amefanya ziara mijini Beijing, Shanghai, Shenzhen na Hongkong. Alisema kampuni ya Canary Wharf ya Uingereza ilisaini makubaliano ya ushirikiano na eneo la Xiong'an mwezi Januari mwaka huu, ili kubadilishana uzoefu wa fedha na huduma na China, na kutoa mchango katika kuunga mkono China kujenga miji yenye teknolojia za kisasa.

    Bw. Bowman tarehe 26 alihudhuria hafla ya uzinduzi wa kituo cha shughuli za fedha zinazotilia mkazo uhifadhi wa mazingira kati ya Uingereza na China mjini Beijing, alisema nchi mbili zitaendelea kutoa mchango kwa maendeleo endelevu ya dunia, kutekeleza ahadi ya kupunguza utoaji wa Carbon Dioxide, kukabiliana na mabalidiko ya hali ya hewa, na kuendeleza uchumi kwa njia isiyochafua mazingira.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako