• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yajaribu njia mpya ya maendeleo kwa kuanzisha eneo la Xiong'an

    (GMT+08:00) 2018-04-01 16:16:16

    Tarehe mosi Aprili mwaka jana, China ilianzisha mji wa Xiong'an, ambao unamaanisha kipindi kipya cha utekelezaji wa sera za mageuzi na ufunguaji mlango nchini China.

    Hivi sasa ujenzi wa mji huo unaendelea kwa utulivu, majengo, na barabara nyingi zimekamilika, reli ya mwendo kasi ya kilomita 350 kwa saa inayounganisha mji huo na Beijing inajengwa. Aidha, makampuni makubwa zaidi ya mia moja yameamua kujenga makao makuu yao mjini humo.

    Hatua iliyopigwa hadi sasa katika ujenzi wa mji wa Xiong'an inaonesha kuwa, njia ya kujiendeleza ya mji huo katika siku za baadaye itakuwa uvumbuzi na mchangayiko, itakuwa juu ya msingi wa mafanikio yaliyopatikana nchini China, na pia itakuwa na umaalumu wa China.  

    Tangu msukosuko wa fedha duniani ulitokea mwaka 2008 na hali hatari ya madeni iliyotokea mwaka 2010 katika Umoja wa Ulaya, China imekuwa injini kuu ya maendeleo ya uchumi wa kimataifa. Watu wanauliza, je, dunia inapaswa kuchagua njia gani ya kujiendelea katika siku za baadaye? Wakati nchi za magharibi zinapokuwa na mashaka huku mfumo na njia zao, CHina ina imani kubwa zaidi kwa chaguo lake.

    Mji wa Xiong'an ni majaribio ya China ya kutafuta njia mpya ya kujiendelea na hata kuendeleza dunia nzima. Ukuaji wa mji huo utashuhudia ustawi wa China na dunia nzima.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako