• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa Somalia azuia mjadala kuhusu hoja ya kutokuwa na imani na spika wa bunge

    (GMT+08:00) 2018-04-01 18:43:32

    Rais wa Somalia Mohamed Abdullahi Farmajo jana amezuia mjadala kuhusu hoja ya kutokuwa na imani na spika wa bunge la nchi hiyo Mohamed Osman Jawari kutokana na hali ya kisiasa nchini humo.

    Akizungumza na waandishi wa habari mjini Mogadishu, Jawari amesema zuio hilo limetokana na mazungumzo kuhusu hoja hiyo, yaliyofanyika siku ya jumamosi kati ya Rais Farmajo, Jawari mwenyewe pamoja na manaibu wake wawili.

    Jawari ambaye anashutumiwa na wabunge wa nchi hiyo kwa kukiuka katiba, alisema Rais aliomba kusimamishwa kwa kikao cha bunge cha jana na pia alitoa wito wa kufanyika mazungumzo kuhusu hali ya sasa ya kisiasa nchini humo, na wote wakakubaliana na ombi hilo.

    Mapema mwezi Machi zaidi ya wabunge 100 walipendekeza hoja ya kutokuwa na imani na Spika wa bunge hilo Mohamed Jawari kwa madai kuwa anakiuka katiba.

    Lakini Jawari ambaye mwaka 2017 alichaguliwa kwa mara ya pili kuwa spika, amemlaumu waziri mkuu wa nchi hiyo Hassan Ali Khaire kwamba ndiye anayechochea kufanyika kwa zoezi la kupiga kura ya kutokuwa na imani na yeye.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako