• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Makubaliano makubwa yafikiwa kati ya Jeshi la Waasi wa Kiislamu na Urusi kuhusu hali ya mji wa Douma nchini Syria

    (GMT+08:00) 2018-04-01 18:45:24

    Makubaliano makubwa yamefanyika baina ya jeshi la waasi na Urusi kuhusu hali ya mji wa Douma nchini Syria, eneo ambalo ndilo lililosalia kwa kushikiliwa na waasi magharibi mwa mji mkuu wa Damascus.

    Kituo cha televisheni cha Alarabiya cha nchini Saudi Arabia kimethibitisha taarifa hiyo iliyotolewa na waangalizi wa haki za binadamu nchini Syria kuwa baada ya mazungumzo yaliyofanyika kwa siku nyingi, Urusi na jeshi la waasi hao wa kiislamu wamefikia makubaliano ya kurejesha hali ya utulivu mjini Douma.

    Kwa mujibu wa taarifa hiyo, sehemu tu ya makubaliano hayo itatangazwa, na sehemu kubwa ikiwa ni kuhusu zaidi kuingia kwa polisi wa Urusi mjini Douma kuwahakikishia raia.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako