• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa Zimbabwe akaribisha wawekezaji kutoka China

    (GMT+08:00) 2018-04-01 18:48:57

    Rais Emmerson Dambudzo Mnangagwa wa Zimbabwe ambaye anatarajiwa kufanya ziara nchini China kuanzia tarehe 2 hadi tarehe 6 mwezi huu amewaambia waandishi wa habari kuwa Zimbabwe inafanya mageuzi na kufungua mlango ili kuvutia uwekezaji na kuhimiza uchumi.

    Rais huyo amesema Zimbabwe itajifunza uzoefu wa maendeleo kutoka China na kuwakaribisha wawekezaji wengi zaidi kutoka China.

    Rais Mnangagwa pia amesema kuwa Zimbabwe itaendeleza uhusiano kati yake na China, kuimarisha mawasiliano kati ya vyama tawala vya nchi hizo mbili, kujifunza uzoefu wa maendeleo kutoka kwa China.

    Na kuhusu pendekezo la Ukanda moja na Njia moja, Mnangagwa amesema ni dhana kubwa ya kukabiliana na mustakabali na litarahisisha biashara ya kimataifa, hivyo Zimbabwe itafanya juhudi kujiunga na mpango huo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako