• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mawaziri wa mambo ya nje wa Misri na Jordan wapinga ukatili wa Israel dhidi ya Wapalestina

    (GMT+08:00) 2018-04-02 08:29:56

    Waziri wa mambo ya nje wa Misri Sameh Shoukry na mwenzake wa Jordan Ayman Safadi wameeleza kupinga vitendo vya kimabavu vya Israel walivyowafanyia waandamanaji wa Palestina hivi karibuni, na kuitaka jumuiya ya kimataifa kubeba wajibu wa kulinda haki za wapalestina.

    Wakiongea kwenye mkutano na wanahabari, mawaziri hao wamesema jumuiya ya kimataifa inapaswa kuwa mstari wa mbele kuwalinda watu wa Palestina na kusukuma mbele juhudi za kuleta amani na kutimiza kile kilichokubaliwa na jumuiya hiyo kuhusu swala hili.

    Takriban Wapalestina 15 wamepigwa risasi na kuuawa na zaidi ya 1,400 kujeruhiwa Ijumaa baada ya vikosi vya Israel kuwafyatulia risasi waandamanaji wa Palestina waliokuwa wakiadhimisha miaka 42 ya siku ya Ardhi na kukusanyika kwenye eneo la mpaka kati ya Ukanda wa Gaza na Israel. Waandamanaji hao wanadai haki ya kurejeshwa wakimbizi wa Palestina waliolazimika kukimbia makazi yao wakati Israel ilipoasisiwa mwaka 1948.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako