• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Libya yafunga zoezi la kuwaandikisha wapiga kura wanaoishi ng'ambo kwa ajili ya uchaguzi ujao

    (GMT+08:00) 2018-04-02 08:41:29

    Tume ya Juu ya Uchaguzi ya Libya jana ilitangaza kufunga zoezi la kuwaandikisha wapiga kura wanaoishi katika nchi za nje kwa ajili ya uchaguzi ujao.

    Kwenye taarifa yake Tume hiyo imetangaza kwa raia wote wanaoishi katika nchi za nje kuwa hadi kufikia Machi 31 mwaka huu mfumo wa uandikishaji kwa wapiga kura wanaoishi nchi za nje umefungwa, ambao uliandikisha wapiga kura 6,630.

    Taarifa pia imeeleza kuwa maombi ya kuandikishwa kupitia balozi mbalimbali za Libya katika nchi za nje pia hayataendelea kupokelewa.

    Tume hiyo hivi karibuni ilitangaza kuwa wapiga kura zaidi ya milioni 2.4 nchini wameandikishwa, ambao wanawakilisha asilimia 50 ya wapiga kura wanaostahiki nchini humo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako