• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Magaidi 22 wa al-Shabaab wauawa Somalia

    (GMT+08:00) 2018-04-02 08:56:01

    Jeshi la Uganda UPDF limesema vikosi vyake jana viliwaua magaidi 22 wa Kundi la al-Shabaab nchini Somalia.

    Katika taarifa aliyoitoa naibu msemaji wa jeshi la UPDF Kalani Deo Akiiki, amesema kikosi kilichoko chini ya Tume ya Umoja wa Afrika nchini Somalia AMISOM, kimewaua magaidi hao wakati walipojaribu kushambulia kambi zilizoko Quoroyole, Buulo Mareer na Golwen katika mkoa wa Lower Shabelle nchini Somalia.

    Taarifa pia imesema, askari wanne wa jeshi la UPDF wameuawa na wengine sita kujeruhiwa katika mapambano hayo yaliyoibuka jana asubuhi. Aidha, magari manane ya wapiganaji yakiwemo mawili yaliyotegwa mabomu yameteketezwa, na kukamata silaha za aina tofauti.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako