• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kundi la Al-Shabaab lawaua viongozi wawili wa wilaya mjini Mogadishu

    (GMT+08:00) 2018-04-02 09:25:44

    Kundi la Al-Shabaab, jana jioni limewaua viongozi wawili wa wilaya mjini Mogadishu nchini Somalia.

    Kwenye taarifa yao kupitia tovuti ya kundi hilo imesema wamewaua maofisa wawili Bw. Hassan Indha-Dhuh na Bw. Mohamud Moallim Hassan Fagase ambao walikuwa viongozi waandamizi wa wilaya ya Hamarweyne iliyoko chini ya utawala wa mkoa wa Banadir.

    Polisi wa Somalia wamethibitisha vifo hivyo, na kusema wanaendelea na uchunguzi ili kuwakamata wapiganaji hao.

    Wakati huo huo, kamanda wa jeshi Bw. Isse Mohamed amesema wamezuia shambulizi la wapiganaji wa Al-Shabaab kwenye kambi ya AMISOM iliyopo Bulamarer, eneo la Lower Shabelle kusini mwa Somalia na wapiganaji kukimbia baada ya kukabiliwa na upinzani mkali wa jeshi la Umoja wa Afrika.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako