• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mji wa London kutoa misaada katika kuijenga Xiong'an wa China kuwa mji wa kisasa "Smart City"

    (GMT+08:00) 2018-04-02 09:49:15

    Wakati uanzishaji wa eneo jipya la Xiong'an la China unapotimia mwaka mmoja, meya wa mji wa fedha wa London wa Uingereza Bw. Charles Bowmanman ametoa makala kwenye Gazeti la Renminribao la China akisema kuwa, mji wake utaunga mkono na kutoa misaada katika kuijenga Xiong'an kuwa mji wa kisasa wa "Smart City" unaoendana na maendeleo ya karne ya 21.

    Bw. Bowmanman amesema mji wa fedha wa London una uzoefu mkubwa katika mipango ya mji, ukusanyaji wa fedha na ujenzi wa miundo mbinu, vilevile una ujuzi na sifa kubwa katika ujenzi wa mji wa kisasa usiochafua mazingira, hali ambayo inawezesha mji huo kushirikiana na China kuhimiza maendeleo ya eneo jipya la Xiong'an.

    Bw. Bowmanman pia ameeleza kuwa juhudi za China katika kuendeleza miji ya kisasa na yenye maendeleo endelevu, pia zimewekwa kwenye pendekezo la "Ukanda mmoja, Njia moja" lililotolewa na rais Xi Jinping wa China. Amesema London inatarajia kushirikiana na China, na kusukuma mbele maendeleo ya "Ukanda mmoja, Njia moja".

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako