• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Klabu bingwa Afrika Mashariki: Mashindano yarejea baada ya miaka miwili, kufanyika jijini Dar es Salaam Tanzania

  (GMT+08:00) 2018-04-02 09:59:05

  Mashindano ya klabu bingwa Afrika Mashariki na kati (CECAFA Club Cup) yanarejea tena mwaka huu baada kupumzika kwa kipindi cha miaka miwili kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo ukosefu wa fedha za uendeshaji.

  Kwa mwaka huu mashindano hayo yatafanyika nchini Tanzania, kuanzia June 30 hadi Julai 14, ambapo klabu za KCCA, GorMahia, Rayon Sports, Simba SC, AZAM FC, LLB, St George na El Hilal zinatarajia kupambana.

  Mashindano hayo yanarejea kwa kile kilichodaiwa kuwa CECAFA imepokea fedha takribani dola za kimarekani milioni 1 kwa ajili ya kuendesha shughuli zake.

  Bingwa wa mwisho katika mashindano ya klabu bingwa alikuwa Azam FC ilipoifunga Gor Mahia mwaka 2015.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako