• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Baada ya Lebron James kuweka rekodi mpya, atabiriwa kuweka nyingine tena

    (GMT+08:00) 2018-04-02 10:01:14

    Wadau wa mchezo wa mpira wa kikapu wameendelea kumpongeza, Lebron James kwa kuweka rekodi mpya ya mchezaji mmoja kufunga zaidi ya pointi 10 kwenye mfululizo wa mechi nyingi za ligi kuu nchini Marekani, ambapo kwenye mchezo wake wa 867 alipofunga pointi 27 wakati timu yake ya Cleveland Cavaliers ilipopata ushindi wa pointi 107-102 dhidi ya New Orleans Pelicans.

    Kwa rekodi hiyo mpya, James anavunja rekodi iliyowekwa na Michael Jordan mwaka 2001 ya kufunga zaidi ya pointi 10 kwenye 866 mfululizo.

    Katika hatua nyingine, James anatabiriwa kuwa huenda akavunja rekodi ya kupata zaidi ya alama 20 kwenye mechi moja ambapo mpaka sasa amefikisha michezo 941 sawa na Kobe Bryant ambaye amestaafu kwa sasa, na rekodi hiyo inashikiliwa na Karl Malone aliyefunga katika mechi 1,134.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako