Kikosi cha Kulina Amani cha Umoja wa Afrika nchini Somalia (AMISOM) kimethibitisha kuwa watu 34 wameuawa wakati wa mapigano makali kati ya kikosi hicho na wapiganaji wa kundi la Al Shabaab kusimi mwa Somalia hapo jana.
Mwakilishi maalum wa mwenyekiti wa kamati ya Umoja wa Afrika kuhusu Somalia, Fransisco Madeira amesema, wapiganaji 30 wameuawa baada ya vikosi vya Umoja huo kuzuia magaidi walioshambulia kambi ya kikosi hicho mkoani Lower Shabelle. Madeira amesema, askari wanne wa AMISOM waliuawa katika mapigano hayo huku wengine sita wakijeruhiwa.
Hata hivyo, kundi la Al Shabaab linadai kuwa wapiganaji wake wamewaua askari 59 wa Uganda katika mapigano hayo.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |