• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania: wafanyibiashara hawapendi agizo la kusafisha mji kwani la wanyima fedha

    (GMT+08:00) 2018-04-02 19:23:39

    Wamiliki wa mikahawa na maduka ya nyama Dar es Salaam wanapoteza kiasi kikubwa cha fedha kwa amri ambayo inawazuia kuufungua biashara kabla ya 9 asubuhi kila Jumamosi ili kutoa nafasi ya kusafisha mji.

    Wamiliki wanaona maelekezo hayo si mazuri kwa biashara na wanataka mamlaka kuchunguza utaratibu, ambao wanadai unawaibia masaa 16 ya kufanya biashara kwa mwezi na karibu saa 200 kwa mwaka.

    Kamishna wa Mkoa Paul Makonda alizindua kampeni ya usafi kwa ajili ya Dar es Salaam mwezi Mei 2016 na akaeleza kwamba hakuna biashara inapaswa kuruhusiwa kufanya kazi kabla ya 9 asubuhi kila Jumamosi ili kuruhusu wakazi kushiriki katika shughuli hiyo.

    Maofisa wa serikali za kaunti wameweka faini ya Sh200, 000 kwa watu waliopatika wa kukiuka maagizo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako