• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Baraza la Usalama la Umoja wa mataifa kuzingatia amani katika vikao vyake vya mwezi huu

    (GMT+08:00) 2018-04-03 09:08:35

    Peru ambayo itakuwa mwenyekiti wa zamu kwa mwezi wa baraza la usalama la umoja wa mataifa, imechagua kuitisha mkutano wa ngazi ya juu kuhusu ujenzi wa amani na ulinzi wa amani.

    Akiongea na wanahabari kuhusu kazi za mwezi huu za baraza la usalama, mjumbe wa kudumu wa Peru katika umoja wa mataifa Bw. Gustavo Meza-Cuadra amesema mkutano huo utaenda sambamba na mkutano wa baraza kuu utakaofanyika Aprili 24 na 25.

    Katika kipindi hicho kutakuwa na mikutano mitatu ya wazi, ikiwa ni pamoja na mkutano kuhusu wanawake, amani na usalama ukizingatia kuzuia unyanyasaji wa kingono kwenye maeneo ya migogoro kupitia uwezeshaji, usawa wa kijinsia na haki.

    Mikutano mingine itahusu vijana, amani na usalama na suala la Palestina na Israel.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako