• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • AU yakaribisha makabidhiano ya madaraka kwa amani Ethiopia

    (GMT+08:00) 2018-04-03 09:42:15

    Mwenyekiti wa Kamati ya Umoja wa Afrika Bw. Moussa Faki Mahamat amekaribisha makabidhiano ya madaraka yaliyofanyika kwa amani nchini Ethiopia, na kuahidi kushirikiana kwa karibu na waziri mkuu mpya Bw. Abiy Ahmed katika sekta mbalimbali za maendeleo.

    Bw. Ahmed aliyeidhinishwa na Bunge la Ethiopia kuwa waziri mkuu mpya wa nchi hiyo, amekabidhiwa madaraka rasmi na Bw. Hailemariam Desalegn aliyejiuzulu tarehe 15 Februari kutokana na maandamano ya kuipinga serikali yaliyotokea nchini humo.

    Bw. Mahamat amesisitiza uungaji mkono wa Umoja wa Afrika kwa ajili ya maendeleo ya Ethiopia na ya Afrika kwa ujumla.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako