• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mwanaharakati wa kupambana na ubaguzi wa rangi wa Afrika Kusini Bibi Winnie Mandela afariki dunia

    (GMT+08:00) 2018-04-03 09:46:18

    Mwanaharakati wa kupambana na ubaguzi wa rangi na aliyekuwa mke wa rais wa Afrika Kusini hayati Nelson Mandela, Bibi Winnie Madikezela-Mandela amefariki dunia katika Hospitali ya Milpark, Johannesburg, Afrika Kusini, baada ya kuugua kwa muda mrefu.

    Bibi Madikizela-Mandela alikuwa mmoja wa watu muhimu katika kupambana na ubaguzi wa rangi. Alipambana kishujaa na serikali ya ubaguzi wa rangi na kupigania uhuru wa nchi.

    Bibi Winnie Mandela anajulikana kama Mama wa Taifa kutokana na kujitoa muhanga kwa ajili ya maslahi ya wananchi wa Afrika Kusini.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako