• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Godfrey Kabera wa Rwanda ashinda ubingwa wa mashindano maalum ya Pasaka

  (GMT+08:00) 2018-04-03 09:56:51

  Godfrey Kabera wa Rwanda ameshinda ubingwa wa Mashindano maalum ya Afrika ya mchezo wa Chess ngazi ya kanda yaliyofanyika katika chuo cha teknolojia cha Kigali nchini Rwanda.

  Mashindano hayo ambayo yaliandaliwa na chama cha mchezo wa Chess cha Rwanda kwa kushirikiana na Chuo cha mafunzo ya mchezo huo cha Afrika Kusini, yalishirikisha wachezaji 32, wakiwemo wawili kutoka Kenya, wawili kutoka Burundi na mmoja kutoka Afrika Kusini

  Mshindi wa pili alikuwa Naftary Wachira kutoka Kenya nafasi ya tatu na ya nne zikitwaliwa na wachezaji kutoka Rwanda.

  Michuano hiyo pia ilitumika kupata timu itakayokwenda kushiriki mashindano ya dunia mwezi Septemba mwaka nchini Georgia.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako