• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Xi Jinping kuhutubia Baraza la Bo'ao kufafanua mustakabali wa mageuzi na ufunguaji mlango wa China

    (GMT+08:00) 2018-04-03 17:29:27

    Mkutano wa mwaka huu wa Baraza la Asia la Bo'ao utafanyika kuanzia tarehe 8 hadi 11 mwezi huu huko Bo'ao mkoani Hainan, China. Waziri wa mambo ya nje wa China Bw. Wang Yi leo ametangaza kuwa, rais Xi Jinping wa China atahudhuria na kuhutubia mkutano huo, na kufafanua mustakabali mpya wa mageuzi na ufunguaji mlango nchini China.

    Katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika leo hapa Beijing, Bw. Wang amesema, licha ya kutoa hotuba kwenye mkutano utakaofanyika huko Bo'ao, rais Xi pia atakutana na viongozi wa nchi na mashirika mbalimbali ya kimataifa watakaohudhuria mkutano huo. Anasema,

    "Huu ni mwaka wa 40 tangu China ianze kutekeleza sera ya mageuzi na ufunguaji mlango, pia ni mwaka wa kwanza tangu kufanyika kwa mkutano mkuu wa 19 wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China. Katika wakati huu muhimu, rais Xi kuhudhuria ufunguzi wa mkutano wa Bo'ao na kukutana na viongozi mbalimbali, kuna maana muhimu katika kusukuma mbele shughuli za kidiplomasia za China katika kipindi kipya, ujenzi wa jumuiya yenye mustakbali wa pamoja, na shughuli za amani na maendeleo za binadamu wote."

    Bw.Wang amesema kwenye mkutano huo, rais Xi atafafanua masuala kadhaa yanayofuatiliwa na jumuiya ya kimataifa, na kutangaza hatua mpya za kuhimiza mageuzi na ufunguaji mlango. Anasema,

    "Mkutano mkuu wa 19 wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China ulitunga mpango mpya wa maendeleo ya China. China itafafanua mawazo, mpango na majukumu yake mapya ya kimaendeleo katika kipindi kipya kwenye mkutano huo."

    Bw. Wang ameeleza kuwa, katika miaka 17 iliyopita tangu Baraza la Asia la Bo'ao lianzishwe, ukubwa na ushawishi wake unapanuka siku hadi siku, na umetoa mchango maalumu kwa ajili ya kukusanya maoni ya pamoja, kuongeza ushirikiano wa kikanda, kuhimiza maendeleo ya pamoja na kutatua masuala ya Asia na dunia. Bw. Wang anasema,

    "Hivi sasa mambo na uchumi wa dunia vinabadilika kwa kina. Nchi mbalimbali duniani zinatafuta njia ya kuhimiza maendeleo ya pamoja huku zikiweza kulinda maslahi yao. Mkutano huo wenye kauli mbiu ya 'Asia inayofungua mlango na kufanya uvumbuzi, na dunia yenye ustawi na maendeleo', unafuata mahitaji halisi, na kufuatiliwa na pande mbalimbali."

    Habari zinasema, viongozi wa nchi na mashirika duniani wakiwemo rais Alexander Van der Bellen wa Austria, rais Rodrigo Duterte wa Philippines, na katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. António Guterres watahudhuria mkutano huo, na kubadilishana maoni kuhusu masuala ya ushirikiano, uchumi na biashara na siasa za kikanda na kimataifa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako