• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mazungumzo ya kibiashara kati ya China na Marekani yapaswa kufanyika kwa msingi wa kuheshimiana na usawa

    (GMT+08:00) 2018-04-03 19:19:04

    Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bw. Geng Shuang leo amesisitiza tena kuwa mlango wa kufanya mazungumzo ya kibiashara na Marekani uko wazi, lakini mazungumzo hayo yanapaswa kufanyika kwa msingi wa kuheshimiana na kutendeana kwa usawa.

    Bw. Geng Shuang amesema, China haitachochea vita vya biashara, haipendi kufanya vita vya biashara, lakini haiogopi vita hiyo, na iko tayari kwa mapambano. Pia amesema, China ina nia na uwezo wa kuchukua hatua zote za lazima, kulinda haki na maslahi yake halali.

    Amesema, China inapenda kutatua migongano ya kibiashara na Marekani kwa njia ya mazungumzo, pia inatumai mazungumzo hayo yanafuata sheria ya kimataifa na kanuni za biashara za kimataifa, wala si sheria ya ndani ya Marekani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako