• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mkutano wa Baraza la biashara kati ya China na Zimbabwe wafanyika Beijing

    (GMT+08:00) 2018-04-03 19:19:45

    Mkutano wa Baraza la biashara kati ya China na Zimbabwe umefanyika leo hapa Beijing na kuhudhuriwa na wajumbe 300 kutoka makampuni ya China, Zimbabwe na maofisa wa ubalozi.

    Rais Emmerson Mnangagwa wa Zimbabwe ambaye yuko ziara hapa China amesema, moja kati ya lengo lake la ziara hiyo ni kupanua ushirikiano wa kibiashara kati ya nchi hizo mbili. Amesema, "Katika miaka ya hivi karibuni China imewekeza kwa kiasi kikubwa kwa ajili ya maendeleo ya uchumi nchini Zimbabwe. Kwa mfano mradi wa kusini mwa Kariba umeifanya Zimbabwe kuzalisha umeme wa megawati 300. Tunaona kuwa maeneo ya ushirikiano yanaweza kuongezeka, na tunapaswa kutafuta fursa mpya za kunufaishana katika sekta za uchumi na biashara. Zimbabwe ina hazina kubwa ya madini, ambayo haijachimbwa vya kutosha. Kwa kuzingatia ufuatiliaji wa wawekezaji wanaotaka kuwekeza nchini kwetu, pia kutia moyo kupanua uwekezaji katika sekta ya uchimbaji madini, serikali yangu imerekebisha kanuni ya zamani ya kujilinda dhidi ya uwekezaji katika sekta hiyo. "

    Takwimu zimeonyesha kuwa, mwaka 2017 uwekezaji wa China nchini Zimbabwe ulizidi dola za kimarekani bilioni 1.8, na thamani ya jumla ya biashara kati ya nchi hizo mbili imefikia dola za kimarekani bilioni 1.3.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako