• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rwanda: Marufuku ya bidhaa za kilimo kutoka Afrika Kusini kuendelea Rwanda

    (GMT+08:00) 2018-04-03 19:23:10

    Serikali ya Rwanda imesema marufuku ya bidhaa za kilimo kutoka Afrika Kusini itaendela kwa muda.

    Marufuku hiyo ilitangazwa na wizara ya kilimo ya Rwanda kutokana na hofu ya ugonjwa wa listeriosis uliozuka Afrika Kusini.

    Ugonjwa huo unaosababishwa na kula chakula chenye viini vya Listeria umeuwa zaidi ya watu 180 nchini Afrika Kusini.

    Mkuu wa Kanuni katika wizara ya kilimo, Beatrice Uwumuremyi, amesema kuwa marufuku hiyo itabaki mpaka serikali ya Afrika Kusini ithibiti ugonjwa huo.

    Rwanda hununua kwa wingi tofaa kutoka Afrika kusini na sasa yameendelea kupungua kutokana na marufuku hiyo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako