• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania: Mradi wa mradi kawi wa mto Rufiji kuanza Julai

    (GMT+08:00) 2018-04-03 19:23:35

    Waziri wa Nishati wa Tanzania Dk Medard Kalemani amesema kuwa hadi kufikia Julai mwaka huu, ujenzi wa bwawa la kuzalisha umeme katika mto Rufiji utakuwa umeanza.

    Ameyasema hayo wakati wa hafla ya kuzindua kituo cha kufua umeme Kinyerezi awamu ya pili.

    Dk Kalemani amesema mradi huo wa miaka mitatu utakamilika kwa wakati.

    Amesema hatua inayoendelea sasa ni kutafuta mkandarasi ambaye hadi kufikia Julai atakuwa ameshapatikana kwa ajili ya kuanza kazi.

    Akizungumzia suala la umeme wa uhakika, Dk Kalemani amesema hadi kufikia mwishoni mwa mwaka huu watakuwa wamekamilisha uimarishaji wa miundombinu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako