• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Spika wa baraza la chini la bunge la Somalia alaani mwito wa kumtaka ajiuzulu

    (GMT+08:00) 2018-04-04 08:51:35

    Spika wa baraza la chini la bunge la Somalia Bw Mohamed Osman Jawari amesema kuwa hatajiuluzu kwa kulazimishwa na serikali, wakati muswada wa kutokuwa na imani naye ukipangwa kujadiliwa leo.

    Akiongea na waandishi wa habari mjini Mogadishu, Bw Jawari amesema kikao kilichopangwa kufanyika leo kujadili mwenendo wake ni haramu na kinakiuka katiba.

    Bw Jawari ambaye amekuwa akilalamikiwa na wabunge kwa kukiuka katiba, yeye pia amemshutumu Rais Mohamed Farmajo kwa kuchochea msukosuko wa kisiasa nchini Somalia kwa kumtaka ajiuzulu, badala ya kutatua msukosuko huo bila kupendelea upande wowote.

    Jumuiya ya kimataifa imesema ina wasiwasi mkubwa kutokana na maendeleo ya saa ya kisiasa na kiusalama nchini Somalia, yanayoweza kuvuruga mafanikio ya kisiasa, kiuchumi na kiusalama yaliyopatikana, na kuchafua sura ya Somalia.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako