• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • AU yasema makabidhiano ya madaraka nchini Ethiopia ni jambo muhimu

    (GMT+08:00) 2018-04-04 08:51:51

    Mwenyekiti wa kamati ya Umoja wa Afrika Bw Moussa Mahamat, amepongeza makabidhiano ya madaraka kwa amani yaliyotokea nchini Ethiopia kuwa ni jambo muhimu kwa Ethiopia na kwa bara la Afrika.

    Akiongea na Waziri mkuu mpya wa Ethiopia Bw. Abiy Mohamed aliyeingia madarakani baada ya kujiuzulu kwa aliyekuwa waziri mkuu wa nchi hiyo Bw. Hailemarian Desalegn kutokana na maandamano ya kuipinga serikali, Bw. Mahamat amesema makabidhiano hayo ya madaraka ni ya kwanza kufanyika kwa amani nchini Ethiopia.

    Bw. Mahamat pia amepongeza mchango muhimu wa Ethiopia katika kuhimiza amani ya kikanda, usalama na mafungamano.

    Viongozi hao pia wamejadili kuhusu ufanisi wa eneo la biashara huru barani Afrika, na kuhusu siasa za ndani ya Ethiopia.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako