• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Katibu mkuu wa UN atoa wito wa kutatuliwa kwa mgogoro wa Yemen njia ya mazungumzo

    (GMT+08:00) 2018-04-04 08:57:10

    Katibu mkuu wa Umoja wa mataifa Bw. Antonio Guterres ametoa wito wa kutatua mgogoro wa Yemen kwa njia ya mazungumzo yanayoshirikisha pande zote. Bw. Guterres amezihimiza pande zinazopambana nchini Yemen ziheshimu sheria za kimataifa, kushirikiana na Umoja wa mataifa, kulinda usalama wa raia na miundombinu ya kiraia, na kutafuta ufumbuzi wa kisiasa wa mgogoro huo uliodumu kwa miaka mitatu. Pia Bw. Guterres ametoa wito kwa Jumuiya ya kimataifa kuchangia fedha kwa ajili ya kuwasaidia watu wa Yemen. Takwimu za Umoja wa mataifa zinasema dola bilioni 3 za kimarekani zinahitajika kutoa misaada ya kibinadamu nchini Yemen kwa mwaka huu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako