• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Hatua ya Marekani na Ulaya kufukuza wanadiplomasia wa Russia yatajwa kuharibu usalama wa Ulaya

    (GMT+08:00) 2018-04-04 08:57:45

    Naibu waziri wa mambo ya nje wa Russia Bw. Alexander Grushko amesema hatua ya hivi karibuni ya Marekani na Ulaya ya kuwafukuza wanadiplomasia wa Russia itaathiri usalama wa Ulaya. Bw. Grushko amesema mshikamano uliooneshwa na baadhi ya nchi za Ulaya katika kuwafukuza wanadiplomasia wa Russia, umezorotesha hali ya usalama barani Ulaya, na kuzuia mawasiliano kati ya Russia na nchi za magharibi, ambayo yana umuhimu mkubwa hasa katika wakati wa msukusuko. Pia amesema umoja kati ya Marekani na washirika wake wa Ulaya umekuwa tishio la moja kwa moja kwa usalama wa Ulaya. Ingawa matokeo rasmi ya uchunguzi kuhusu jasusi wa zamani wa Russia kuwekewa sumu nchini Uingereza hayajatolewa, mzozo wa kidiplomasia unaotokana na tukio hilo umeendelea kupamba moto, na mpaka sasa nchi za magharibi zimewafukuza wanadiplomasia zaidi ya 150 wa Russia.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako