• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Marais wa China na Zimbabwe wakutana Beijing

    (GMT+08:00) 2018-04-04 09:28:45

    Rais Xi Jinping wa China amefanya mazungumzo na mwenzake wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa ambaye yuko ziarani nchini China.

    Viongozi hao wamekubaliana kuinua kiwango cha uhusiano kati ya China na Zimbabwe kufikia ngazi ya uhusiano wa wenzi wa kimkakati.

    Kwenye mazungumzo yao, rais Xi Jinping amesema katika muda mrefu uliopita, serikali na vyama vya nchi hizo mbili vimekuwa vikidumisha uhusiano wa karibu, pande hizo mbili zimekuwa zikiheshimiana, kutendeana kwa usawa, kudumisha kiwango cha juu cha kuaminiana kisiasa, na kuimarisha ushirikiano wa kiuchumi na kibiashara na mawasiliano ya kiutamaduni.

    Kwa upande wake rais Mnangagwa amesema Zimbabwe siku zote inashikilia sera ya kuwepo kwa China moja. Amesisitiza kuwa Zimbabwe itaendelea na juhudi za kukuza uhusiano kati yake na China, kuunga mkono ushirikiano unaofanyika chini ya mfumo wa Baraza la ushirikiano kati ya China na Afrika, na kuunga mkono ushiriki wa Afrika kwenye ujenzi wa "Ukanda mmoja, Njia moja".

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako