• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yajiandaa kuchukua hatua kujibu hatua za kujilinda kibiashara za Marekani

    (GMT+08:00) 2018-04-04 09:29:31

    Ofisi ya mwakilishi wa biashara wa Marekani imetoa taarifa ikitangaza orodha ya bidhaa za China zitakazoongezwa ushuru wa forodha kwa mujibu wa matokeo ya ripoti kuhusu ukaguzi wa kipengele cha 301 cha sheria ya biashara, ambazo zinahusisha bidhaa zenye thamani ya dola za kimarekani bilioni 50 zinazoagizwa kutoka China kwa mwaka.

    Taarifa hiyo imependekeza kuongeza ushuru wa forodha kwa asilimia 25 kwa bidhaa za aina 1,300 zinazoagizwa kutoka China, ambazo zinahusisha sekta za TEHAMA, usafiri wa anga na anga za juu, roboti, matibabu na dawa, na mashine.

    Akizungumzia hatua hiyo ya Marekani, msemaji wa Wizara ya biashara ya China ametangaza kuwa China inapinga kithabiti hatua hiyo ya Marekani, na kuitaja kuwa imekiuka vibaya kanuni za kimsingi za WTO, na kwamba China inajiandaa kuwasilisha malalamiko kuhusu hatua hiyo ya Marekani kwenye Baraza la kusuluhisha migogoro la WTO. Pia amesema China itachukua hatua madhubuti za kujibu hatua hiyo ya Marekani na itazitangaza hivi karibuni.

    Msemaji huyo amesisitiza kuwa China ina imani na uwezo wa kukabiliana na hatua yoyote ya kujilinda kibiashara ya Marekani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako