• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • CAF yatuma taarifa kwa Yanga na Wolaitta kutotumia baadhi ya wachezaji

    (GMT+08:00) 2018-04-04 10:50:03

    Shirikisho la soka barani Afrika (CAF) jana kutoka makao makuu ya shirikisho hilo mjini Cairo Misri limetoa taarifa rasmi kwa vilabu vya Yanga SC ya Tanzasnia na Wolaitta Dicha SC ya Ethiopia kuhusu wachezaji ambao vilabu hivyo haviruhusiwi kuwatumia.

    CAF wametuma taarifa inayoiwazuia Yanga kuwatumia wachezaji wake wanne ambao ni Kelvin Yondani, Obrey Chirwa, Papy Tshishimbi na Sidi Juma, huku timu ya Ethiopia imezuiwa kuwatumia wachezaji wake wawili kutokana na kutumikia kadi za njano.

    Timu hizo zitakutana katika mchezo wa kwanza wa mtoano wa kuwania kuingia hatua ya makundi ya kombe la shirikisho Afrika jijini Dar es Salaam kati ya April 6 au 8 mwaka huu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako