• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yaongeza ushuru kwa bidhaa za Marekani zenye thamani ya dola bilioni 50

    (GMT+08:00) 2018-04-04 16:36:36

    China leo imetoa orodha ya bidhaa zenye thamani ya dola za kimarekani bilioni 50 zilizoagizwa kutoka Marekani ambazo zitaongezewa ushuru, ikiwemo soya, magari na bidhaa za kemikali.

    Wizara ya Fedha ya China imeandika kwenye tovuti yake kuwa, Tume ya Ushuru wa Forodha iliyo chini ya Baraza la Serikali la China imeamua kuweka ushuru zaidi wa asilimia 25 kwa bidhaa 106 zilizo chini ya vifungu 14.

    Hatua hiyo imechukuliwa baada ya utawala wa Marekani kutangaza pendekezo la orodha ya bidhaa zitakazoongezewa ushuru, ambazo zinahusu bidhaa zinazosafirishwa na China zenye thamani ya dola za kimarekai bilioni 50, huku ukipendekeza ushuru wa kiwango cha asilimia 25.

    Wizara hiyo imesema, utekelezaji wa hatua hiyo unategemea na lini serikali ya Marekani itweka ushuru kwa bidhaa za China.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako