• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kama Trump akitaka kutoza ushuru mkubwa wa adhabu, hakika atahatarisha maslahi ya Marekani

    (GMT+08:00) 2018-04-04 17:44:45

    Ofisi ya mwakilishi wa biashara wa Marekani imetoa taarifa ikitangaza orodha ya bidhaa za China zitakazoongezwa ushuru wa forodha, ambazo zinahusisha bidhaa zenye thamani ya dola za kimarekani bilioni 50 zinazoagizwa kutoka China kwa mwaka.

    Kwa mujibu wa taarifa hiyo, orodha hiyo iliyotolewa baada ya mahesabu kwa mfumo wa kompyuta, itaongeza kwa kiasi kikubwa gharama kwa wafanyabiashara wa China na kulinda zaidi maslahi ya wazalishaji wa Marekani. Lakini orodha hiyo ikiangaliwa kwa undani, inaonekana kuwa Marekani inafanya kazi bure ambayo inadhuru maslahi ya wengine, na wala haisaidii maslahi yake yenyewe.

    Baadhi ya bidhaa za madini zilizowekwa kwenye orodha hiyo kama thorium alloy, Depleted uranium alloy, kauri inayohimili joto kali na nyingine, bidhaa zisizotakiwa kuuzwa Marekani. Bidhaa hizo zinaleta uchafuzi wakati zinapotengenezwa, inapaswa kuwekewa vizuizi kuuzwa nje, vilevile, baada ya China kujiendeleza, mahitaji yake kwa bidhaa hizo pia yataongezeka, kwa hivyo vikwazo vya Marekani dhidi ya bidhaa hizo si jambo baya kwa China.

    Bidhaa za chuma cha pua na Aluminum za China haziuzwi kwa wingi nchini Marekani. Kama serikali ya Marekani inafikiri hali yake ya kisiasa na kulinda sekta yake ya madini ya metali, haitoshi kuzuia China tu. Kutokana na hali ilivyo sasa, Rais Trump anasamehe wafanyabiashara wa nchi nyingine waliowekewa vikwazo zamani, China inaelewa sababu yake ya kisiasa ya kuzingatia washirika wake na kutaka kushirikiana nao kufanya vita vya biashara dhidi ya China kwa pamoja, lakini hatua hizo haitakuwa na ufanisi katika kulinda sekta yake ya ufuajiwa metali.

    Na bidhaa mbalimbali za mashine pia zimewekwa kwenye orodha ya kuongezwa ushuru, na nyingi kati yake ni bidhaa za maisha ya kawaida ya watu wa Marekani. Watu wa kawaida wa Marekani wana mahitaji makubwa kwa genereta ndogo, vifaa vya kutumia umeme na vifaa vingine. Lakini Marekani haina viwanda vya kutengeneza vifaa hivyo, na pia bei zake ni ghali. Migongano ya kibiashara hakika utafanya gharama za maisha kwa watu wa kawaida wa Marekani kuongezeka.

    China imejibu kuwa itachukua hatua kali zinazolingana na zilizochukuliwa na Marekani. Kwa mujibu wa makadirio ya nje, hatua hizo za China huenda zitaleta maumivu kwa Marekani. Hatua hizo siyo tu zitakuwa tatizo lingine kubwa kwa uchumi wa Mareknai, lakini huenda zitaharibu hali ya kisiasa ya serikali ya Trump.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako