• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yasema hakuna mshindi katika mkwaruzano wa biashara

    (GMT+08:00) 2018-04-04 17:55:48

    Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bw. Geng Shuang leo amesema, hakuna mshindi katika mkwaruzano wa biashara, na China inatumai Marekani itaacha msimamo wa upande mmoja na hatua za kujilinda kibiashara, kurudi kwenye njia sahihi ya mazungumzo na ushirikiano wa kunufaishana.

    Bw. Geng Shuang amesema: "Hakuna mshindi katika mkwaruzano wa biashara, mzusha vita atadhuru maslahi ya wengine na yake mwenyewe. Hatua ya Marekani kwanza inadhuru maslahi yake yenyewe. Tumeona kuwa sekta ya biashara ya Marekani, watu wa kawaida wa Marekani, vyombo vya habari na washauri bingwa wana wasiwasi kuhusu matokeo mabaya yanayosababishwa na hatua hiyo, nchi mbalimbali na mashirika ya kimataifa pia wanafuatilia na kupinga hatua hizo za upande mmoja na kujilinda kibiashara. Tunatumai Marekani kusikiliza kauli hiyo, kuacha hatua zisizo sahihi na kurudi kwenye njia sahihi ya mazungumzo na ushirikiano wa kunufaishana."

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako