• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yaanza rasmi utaratibu wa kutatua mgogoro wa biashara na Marekani kupitia WTO

    (GMT+08:00) 2018-04-04 19:47:36

    Wizara ya biashara ya China leo imesema, China imetoa ombi la kufanya mazungumzo, na kuanza rasmi utaratibu wa kutatua mgogoro wa biashara na Marekani kupitia Shirila la Biashara Duniani WTO.

    Hatua hiyo imekuja baada ya Marekani kupendekeza kuongeza ushuru wa forodha kwa bidhaa za China kwa mujibu wa ukaguzi wa kipengele cha 301 cha sheria ya Marekani dhidi ya China.

    Wizara hiyo imesema Marekani inapuuza kanuni za WTO, na kukiuka ahadi zake kwa shirika hilo, kwa kupendekeza kuongeza ushuru wa forodha kwa asilimia 25 kwa bidhaa zinazoagizwa kutoka China zenye thamani ya dola za kimarekani bilioni 50. Kitendo hicho si kama tu kimedhuru maslahi halali ya China, bali pia kimekiuka kanuni za WTO, na kitadhoofisha mfumo wa pande nyingi wa biashara uliojengwa kwa mujibu wa kanuni za WTO.

    Wizara hiyo imesema China inaamini kuwa mamlaka ya kutatua migogoro ya biashara ya WTO itashughulikia jambo hilo kwa haki na kufuata hali halisi, ili kulinda utaratibu wa kimataifa wa biashara.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako