• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yasema haitarudi nyuma kutokana na shinikizo inayotolewa na upande wowote

    (GMT+08:00) 2018-04-04 20:39:50

    Marekani leo imetoa orodha ya bidhaa zitakazoongezewa ushuru wa forodha, na kupanga kuongeza ushuru wa forodha kwa asilimia 25 kwa bidhaa za aina 1,333 zenye thamani ya dola za kimarekani bilioni 50. Ili kujilinda, serikali ya China leo imeamua kuongeza ushuru wa forodha kwa asilimia 25 kwa bidhaa za aina 106 zinazoagizwa kutoka Marekani. Ofisa waandamizi wa wizara ya fedha na wizara ya biashara za China wamesema, China haitarudi nyuma kutokana na shinikizo la nje, na kama kuna mtu akitaka kufanya vita ya biashara, China haitarudi nyuma hata kidogo.

    Naibu waziri wa biashara wa China Bw. Wang Shoucheng amesema, hatua ya Marekani ya kuongeza ushuru wa forodha kwa bidhaa za China imekiuka wajibu wa kimataifa wa Marekani. Anasema,

    "Kutokana na sheria za kimataifa na kipengele cha 7 cha sheria ya biashara ya kimataifa ya China, China ni lazima ilipize kisasi hatua ya nchi yoyote ya kuibagua China katika shughuli za biashara. Hivyo China imetangaza orodha ya kuongeza ushuru wa forodha kwa bidhaa za Marekani zenye thamani ya dola za Kimarekani bilioni 50."

    Naibu waziri wa fedha wa China Bw. Zhu Guangyao amesema, China imeweka soya kutoka Marekani katika orodha hiyo kutokana na matakwa ya wakulima wa China. anasema,

    "Kusema kweli, China inaagiza asilimia 60 ya soya ya Marekani inayouzwa katika nchi za nje. Wakulima wa China waliishtaki Marekani kutoa ruzuku kwa wakulima wao wa soya, kitendo hicho kimedhuru maslahi ya wakulima wa China. Lakini hadi sasa orodha ya China haijatekelezwa, sasa ni wakati wa kufanya mazungumzo."

    Alipozungumzia wasiwasi wa Marekani kuhusu "mpango wa mwaka 2025 wa uzalishaji wa China", Bw. Wang Shouwen amesema mpango huo unafuata kanuni ya WTO, na ni wa wazi na dhahiri na hauna ubaguzi wowote, China inakaribisha makampuni duniani kushiriki kwenye mpango huo.

    Kwenye mkutano na waandishi wa habari uliofanyika leo, maofisa waandamizi wa wizara ya fedha na wizara ya biashara za China wote wamesema, China haipendi kujipatia urari mzuri, na kutaka kutimiza uwiano wa biashara kupitia ushirikiano. Hakuna mshindi katika mvutano wa kibiashara, ikiwa mwanachama anayejiwajibisha wa WTO, China haipendi kuwepo kwa mvutano huo, lakini haiogopi mvutano huo.

    Naibu waziri wa fedha wa China Bw. Zhu Guangyao amesema, China itatoa hatua mpya za mageuzi, na kuufungua mlango zaidi katika siku za baadaye.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako