• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mgogoro wa kibiashara kati ya China na Marekani waathiri bidhaa za kilimo katika jimbo la Oregon

    (GMT+08:00) 2018-04-05 08:47:55

    Mvutano kuhusu ushuru wa forodha kati ya China na Marekani, unaoonekana kuzusha mgogoro wa kibiashara kati ya nchi hizo mbili, utakuwa na athari kwa bidhaa za kilimo katika jimbo la Oregon la pwani ya magharibi ya Marekani.

    Gazeti la Register Guard la Oregon limesema kutakuwa na madhara kama China itaendelea kutekeleza uamuzi wa kutoza ushuru wa asilimia 25 kwa bidhaa za kilimo zinazotoka katika jimbo hilo. Mkurugenzi wa idara wa kilimo ya jimbo hilo Bw Alexis Taylor amesema hatua hiyo itakuwa na madhara kwa jimbo hilo.

    China ni mwagizaji mkubwa wa nne wa bidhaa za kilimo kutoka Oregon, mwaka jana peke yake iliuza bidhaa hizo kwa China zenye thamani ya dola za kimarekani milioni 320.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako